Zanzibar Business And Property Registration Agency

Company Registration

Kampuni inaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti, kwa urahisi ni mkusanyiko wa watu wawili au zaidi walioamua kuunda taasisi ya kisheria inayounganisha rasilimali zao ikiwa ni pamoja na mali na ujuzi wao kwa lengo la pamoja la kufanya biashara itakayowapatia faida.
Kampuni inatambulika kisheria pale tu inapokuwa imesajiliwa kwa mujibu wa sheria zinazohusika. Sheria ya Kampuni (The Companies Act No. 15 of 2013) ndiyo inayoongoza usimamizi na uendeshaji wa kampuni zinazofanya shughuli zake Zanzibar.

Kampuni zinaweza kutofautishwa kwa kutegemea vigezo mbalimbali, miongoni mwao ni kama ifuatavyo:-

(a) Kampuni binafsi (Private Companies)

Kwa kawaida kampuni binafsi huundwa na watu wenye uhusiano kabla ya uhusiano wao wa kibiashara, kama vile baba, mama, motto, rafiki n.k
• Idadi ya wajumbe si chini ya wawili na wasiozidi hamsini bila ya kujumuisha waajiriwa.
• Hisa za kampuni zinahamishwa kwa masharti maalum.
• Ni marufuku kualika uma kununua hisa zake.

(b) Kampuni za Umma (Public Companies)

Kampuni hizi hazina ukomo wa idadi ya wajumbe ila wasiwe chini ya saba.
• Mtu yoyote anaweza kununua hisa za kampuni ya Umma katika soko la hisa na kuwa mjumbe wa kampuni.
• Kampuni za umma zinalazimika kutoa tangazo au mualiko kwa umma ili waweze kununuwa hisa. Mualiko huo hufanywa kupitia waraka wa hisa ‘Prospectus’ ambao unapaswa kuelezea malengo ya kampuni, mtaji wa hisa unaopendekezwa, chanzo cha fedha na matajio ya kampunikwa jumla.
• Kampuni binafsi inaweza kubadilishwa na kuwa kampuni ya umma.
• Kampuni za umma zinalazimika kuwa na katiba na kanuni zilizoandaliwa kwa umakini ili kuhakikisha inakuwa na uhusiano mzuri baina ya wajumbe, wakurugenzi na wadau wengine.

(c) Kampuni zenye ukomo wa dhima (Limited Liability Companies)

Wajumbe wa kampuni za aina hii wanakuwa na dhima yenye ukomo kwa mujibu wa katiba ya kampuni, ambapo inaweza kuwa ukomo wa hisa au wa dhamana.

(d) Kampuni ya ukomo wa hisa

Dhima ya wajumbe inawekwa kama kima ambacho hakikulipwa kwenye hisa zinazomilikiwa na kila mmoja wao; au
(e) Kampuni ya ukomo wa dhamana
Dhima ya wajumbe inawekwa kwa kiasi ambachoi wajumbe wanaweza kuchangia kwenye rasilimali za kampuni itokeapo kampuni kufungwa.

(f) Kampuni zisizokuwa na ukomo (Unlimited Companies)

Kampuni ambazo hazina ukomo juu ya dhima ya wajumbe wake, ikiwa itatokea kampuni kufungwa wajumbe watakuwa na dhima juu ya madeni yote ya kampuni.

(g) Kampuni za kigeni (Foreign Companies)

• Hizi ni kampuni zilizoundwa na kusajiliwa nje ya Zanzibar.
• Ofisi zao za Zanzibar zinajulikana kama matawi ya kampuni za kigeni. Hata wajumbe au wanahisa wote ni Wazanzibari, kampuni itaonekana ni ya kigeni.
Usajili wa kampuni

Kampuni husajiliwa kwa utaratibu ufuatao:-

(a) Waomabaji wanaweza kuwasilisha maombi kwa barua au kufika wenyewe katika ofisi za usajili kwa ajili ya ukaguzi wa jina lkatika daftari la usajili.
(b) Waombaji wanashauriwa juu ya upatikanaji wa jina ili waweze kuandaa katiba na kanuni za kuiwasilisha kwa ajili ya usajili.
(c) Uwasilishaji wa vielelezo vya usajili

i. Katiba na kanuni za kampuni zilizosainiwa na wajumbe mbele ya shahidi (angalau nakla tatu)
ii. Anuani kamili za ofisi ya kampuni
iii. Kiapo cha utii wa masharti ya sheria
iv. Taarifa za wakurugenzi na katibu wa kampuni n.k

(d) Usajili wa kampuni za kigeni unafanywa baada ya kuwasilisha:-

i. Nakala zilizothibitishwa za katiba na kanuni za kampuni.
ii. Nakala ya hati ya kuundwa kampuni.
iii. Notisi ya mahala ilipo ofisi ya kampuni iliyosainiwa katika nchi iliyoundwa.
iv. Orodha ya wakurugenzi wa kampuni.
v. Orodha ya wawakilishi wa kampuni nchini.
vi. Uthibitisho kwamba kampuni ipo hai.

Kuna aina tatu ya ada inayolipwa na waombaji kwa ajili ya usajili wa kampuni
1. Ada ya usajili
Sh. 2,800/= kwa milioni moja ya kwanza ya mtaji wa kampuni.
Sh. 2,000/= kwa milioni moja ya pili na
Sh. 1/= kwa kila sh. 1,000/= iliobaki (0.1%) katika mtaji wa kampuni.
2. Ada ya kufaili
Sh. 5,000/=
3. Ushuru wa stempu
Sh. 50,000/= kwa katiba ya kampuni.
Sh. 50,000/= kwa kanuni za kampuni
1% asilimia moja ya mtaji wa kampuni kwa kiwango kisichozidi sh.100,000/=

(a) Kampuni zote zinatakiwa kuwasilisha taarifa za marejesho ya mwaka ambayo inafanywa katika fomu maalum. Taarifa za ukaguzi ni sehemu ya marejesho. Kampuni za kigeni wanatakiwa faili tu.
(b) Malipo yote yanalipwa kwa Mrajis wa Kampuni ambapo risiti hotolewa. Waombaji wanashauriwa kuondokana na kufanya malipo ambayo hayatolewi risiti.
(c) Mabadiliko yoyote yanayotokea katika kampuni lazima yatolewe taarifa kwa Mrajis/ Msajili mara moja. Mrajis baada ya kubainisha taarifa atabadilisha katika daftari la usajili baada ya kufanywa malipo ya kufaili taarifa hizo. Adhabu itatolewa iwapo mabadiliko hayakutolewa taarifa kwa wakati.
(d) Kampuni baada ya mwaka mmoja imeshindwa kufanya shughuli zake kwa sababu yoyote ile, maafisa wake wanaweza kumuarifu Mrajis ambaye ataifuta kampuni hiyo kwenye daftari la usajili.
(e) Iwapo hakuna taarifa iliyotolewa, Mrajis ataamini kampuni inaendelea na biashara na itatakiwa kutekeleza mahitaji yote ya kisheria ya kuendesha kampuni.

OUR PARTNERS
USER GUIDE FOR ORSZ
Firm
Company
Documents
About Us
Contact Us
CONTACT US
USER GUIDE FOR ORSZ
Firm
Company
Documents
About Us
Contact Us

©2023 - Zanzibar Business and Property Registration. Developed by: CMB

Terms and Conditions / Privacy and Policy