Zanzibar Business And Property Registration Agency

Documents Registration

Waraka ni karatasi yenye maandishi ambayo imekusanya taarifa zilizowekwa kwa malengo ya matumizi maalumu na kutumika kama kumbukumbu kwa ajili ya matumizi ya baadae. Nyaraka husajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Nyaraka Sura ya 99, Sheria ya Zanzibar (Document Registration Decree Cap. 99 of 1919).

Kuna aina nyingi za nyaraka kwa misingi ya usajili, nyaraka zimegawika katika sehemu nne (4) zifuatazo:
1. Waraka wa mikopo (Mortgage Deed) A-1
Aina hii ya waraka inajumuisha
• Mikopo baina ya mtu binafsi na benki au taasisi yoyote ya kifedha (hujulikana kama rehani –mortgage)
• Mikopo baina ya kampuni na benki au taasisi nyengine za fedha (aina hii hujulikana kama stakabadhi za mikopo – Debenture)
2. Waraka wa mauziano A-2
Hii ni aina ya nyaraka inayojumuisha waraka wa mauziano (sale deed) na mirathi (beneficiary)
3. Mikataba A-3
Nyaraka za aina hii zinajumuisha Wakfu (Wakf deed) mikataba ya kukodishana (lease agreement), kiapo cha umiliki (statutory declaration), hiba (gift) na aina yoyote ya mikataba halali inayofungwa Zanzibar.
4. Waraka wa kufuta deni A-4
Ni waraka unaotayarishwa baada ya deni kumaliza kulipwa (discharge of mortgage or debenture)
Hatua na utaratibu wa kusajili Nyaraka

i. Muombaji huwasilisha waraka ulioandaliwa kwa mujibu wa sharia na vigezo vinavyoainishwa na Mrajis wa Nyaraka (waraka unawea kutengenezwa na mtu yoyote mwenye uwezo na sifa; mfano taasisi za kishauri (consultant firms), taasisi za kisheria, wakili na BPRA au wataalamu wengine wenye sifa za kuandaa waraka kwa kutegemea aina ya waraka wenyewe)
ii. Kuwasilisha vielelezo muhimu vinavyohusiana na waraka vikiwmo;
• Vitambulisho vinavyotambuliwa na Serikali
• Vielelezo vya umiliki wa mali
• Barua ya Sheha wa shehia iliopo mali husika n.k
iii. Kulipa ada katika kusajili waraka, muombaji anatakiwa kulipa ada za usajili kama ifuatavyo:
• Ada ya usajili Sh. 20,000/=
• Ada ya kuandaa waraka 20,000/= (kwa waraka unaoandaliwa na BPRA tu)
• Ushuru wa stempu
2% (asilimia mbili) ya thamani ya waraka (kwa mauziano, wakfu, hiba n.k)
1% (asilimia moja) ya thamani ya waraka usiozidi zaidi ya Sh. 100,000/= (kwa stakabadhi za mikopo na rehani)
Sh. 10,000/= (kwa viapo vya umiliki, wasia na mikataba mengineyo).
iv. Kukamilisha usajili
Usajili hukamilika kwa mkataba kutiwa saini na Mrajis.

i. Kutambulika mbele ya sheria
ii. Kuepusha utata na mizozo inayoweza kutokea (kutokana na waraka kuewkwa kwa maandishi)
iii. Kuimarisha ushahidi unaotambulika kisheria katika makubaliano, umiliki wa mali na mikataba mengine n.k
iv. Kuondosha utata juu ua mmiliki halali wa mali husika, better tittle.
v. Kuwa na kumbukumbu imara, na wa kudumu endapo itatokezea waraka kupotea, kuungua, kuibiwa n.k nakala inayobaki BPRA hutumika kama marejeo.

i. Kukosa ushahidi wa moja kwa moja (direct evidence)
ii. Uwezekano wa kuleta utata wakati wa kutaka kuuza mali hiyo au mmiliki anapofariki.
iii. Kukosekana kumbukumbu kwa kizazi kijacho juu ya mali husika.
iv. Kupoteza sifa za kupata mkopo kutoka benki au taasisi nyengine za kifedha.
v. Kushindwa kuitumia mali kama dhamana (Bail) endapo nyaraka haikusajiliwa.

OUR PARTNERS
USER GUIDE FOR ORSZ
Firm
Company
Documents
About Us
Contact Us
CONTACT US
USER GUIDE FOR ORSZ
Firm
Company
Documents
About Us
Contact Us

©2023 - Zanzibar Business and Property Registration. Developed by: CMB

Terms and Conditions / Privacy and Policy